Fredwaa aagwa Dar, kuzikwa kesho Sanya Juu

0
170

Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa vituo mbalimbali vya habari hapa nchini Fredy Fidelis Maarufu FREDWAA, umeagwa hii leo katika kanisa la Mtakatifu Gasper Mbezi Beach mkoani Dar es salaam.

Baadhi ya Watangazaji na Waandishi wa habari waliowahi kufanya kazi na marehemu Fredwaa wamemuelezea kuwa alikuwa mwalimu na mtangazaji wa aina yake hapa nchini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tido Mhando amemueleza Marehemu Fredwaa kuwa alikuwa ni mtangazaji aliyekuwa na haiba ya peke yake na alifanya kazi zake kwa weledi.

Fredwaa aliyefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari eneo la Kawe mkoani Dar es salaam, ameacha Mjane na Watoto wawili na anatarajiwa kuzikwa hapo kesho nyumbani kwao Sanya Juu wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.