FCC watakiwa kulinda bidhaa zinazozalishwa nchini

0
147

Waziri wa Viwanda na Biashara profesa kitila Mkumbo ameitaka tume ya ushindani nchini – FCC kuweka mazingira mazuri ya udhibiti wa ushindani wa Biashara nchini Kwa lengo la kumlinda mlaji na bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Profesa Mkumbo ametoa muongozo huo wakati akifungua mkutano wa Tano wa majadiliano ya mpango mkakati wa FCC utakaoiwezesha tume hiyo kuweka mazingira Bora ya ushindani kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.

Awali akimkaribisha waziri Mkumbo, naibu katibu Mkuu wa wizara hiyo Exaud Kigahe ameiyaka FCC kuweka mazingira Bora ya kuamua migogoro ya kibiashara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa tume ya ushindani (FCC) William Erio ameelezea lengo la mkutano huo kuwa ni kuweka mpango mahususi wa kusimamia ubora wa huduma na kumlinda mlaji.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine utaiwezesha FCC kuwa na mpango Bora wa kuamua mashauri mbalimbali ya kibiashara na kusimamia ushindani hapa nchini