Fanyeni kazi, hakuna cha bure : Kauli ya Rais Magufuli

0
242

Rais John Magufuli amerejea kauli yake ya kuwataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo.

Akizungumza na Wakazi wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora akiwa njiani kuelekea mkoani Shinyanga, Rais Magufuli amesema kuwa, mtu yeyote asitegemee fedha ya bure pasipo kufanya kazi.

Amesema kuwa kwa upande wake Serikali itahakikisha inapeleka huduma zote muhimu katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na afya, maji na umeme ili kuwawezeshesha Wakazi wa maeneo hayo kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, wakati wa mtu kusubiri ili apatiwe msaada na Serikali ama kupata fedha ya bure umepita, hivyo ni lazima kujituma kufanya kazi itakayowezesha kujipatia kipato.