Familia yataka waliomuua ndugu yao kukamatwa

0
148

Mkazi wa Kijiji cha Kisesa, Kata ya Imalamate wilayani Busega mkoani Simiyu, Sospiter Kanyanga ameiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria watu waliohusika na kifo cha mwanaye, Tabu Sospiter aliyeuawa Machi 30 mwaka huu akiwa shambani.

Akizungumza na TBC, Kanyanga amedai kuwa watu waliomuua mwanaye na kisha kuufukia mwili wake chini ya mti wanafahamika vyema kijini hapo na tayari ameshawasilisha majina yao polisi na kueleza kushangazwa na kigugumizi cha kuwatia mbaroni.

Mwili wa Tabu uliokotwa kwenye shamba la viazi la ukweni kwake Aprili 3, mwaka huu ukiwa umefukiwa chini ya mti.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Richard Abwao amesema uchunguzi bado unaendelea.