Diwani wa Kata ya Lupaso mkoani Mtwara, Douglas Mkapa amesema kuwa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alikuwa na mpango wa kujenga kituo cha afya pamoja na kujenga mradi wa maji kutoka Mto Ruvuma.
Akizungumza na TBC mapema leo nyumbani kwa Mzee Mkapa, kijijini Lupaso, diwani huyo amesema tayari walikuwa wametenga eneo lenye ukubwa wa hekari 30 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.
Kufuatia kifo cha Mzee Mkapa, Douglas ambaye ni mtoto wa mdogo wa Rais huyo wa awamu ya tatu amesema anaamini serikali itaendeleza miradi hiyo iliyolenga kuboresha maisha ya wakazi wa Kijiji cha Lupaso.
Aidha, amesema anatamani kuona serikali ikifanya nyumbani kwa Rais Mkapa kuwa eneo la makumbusho ambapo watu wataweza kutembelea na kujifunza kuhusu maisha yake.