Familia kushirikishwa kwenye mazishi ya ndugu zao

0
491

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi amewaelekeza maafisa afya na waganga wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuhakikisha familia zinashirikishwa kikamilifu na bila hofu katika kuandaa na kufanya mazishi ya ndugu na jamaa zao waliofariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa corona.

Profesa Makubi ametoa maelekezo hayo jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya serikali kwa umma kuhusu mapambano yanayoendelea dhidi ya virusi vya corona.