Falsafa ya KAZEN yapigiwa chapuo kukuza viwanda nchini

0
171

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amefungua Kongamano la tatu la wakufunzi la KAIZEN lilioandaliwa na Kitengo cha KAIZEN kilichopo Wizara ya Viwanda na Biashara.

Akifungua mkutano huohii leo Dkt. Hashil Abdalllah amesema anaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwezesha Kongaano la KAIZEN lililofanyika mwaka huu nchini Tanzania na pia ameishukuru serikali ya Japan kupitia JICA kuendelea kufadhili mradi huo.

Dkt. Hashil ameongeza kwa kusema kuwa “Falsafa ya KAIZEN inasaidia kuongeza Tija, Ufanisi, Ubora na pia kuongeza fulsa za ajira, Falsafa hii imesaidia kubadilika kwa mtazamo na fikra kwa wamiliki wengi wa Viwanda inayopelekea kukua kwa biashara zao” Amesema Dkt. Hashil.

Ameongeza kwa kusema kuwa viwanda 135 tu ndio vilivyofikiwa na KAIZEN hivyo amewataka wakufunzi walioshiriki kongamano hili kujadiliana kwa kina kuona namna bora ya kuvifikia viwanda vingi zaidi vilivyopo nchini.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwanda, Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Lugano Wilson Amesema kuwa kama ilivyo katika nchi nyingi duniani, ni jukumu la Serikali kuweka mazingira bora ya biashara ambayo yatachangia kuifanya nchi kuwa ya ushindani zaidi katika uzalishaji, biashara na shughuli nyinginezo za kiuchumi ili kutambuliwa kama nchi ya ubora, ufanisi na tija.

Naye mwakilishi kutoka shirikisho la wenye Viwanda nchini Tanzania (CTI) Neema Mhando Ameipongeza wizara ya viwanda na biashara kwa kutekeleza falsafa ya KAIZEN kwa vitendo na kwa mafanikio makubwa.