Faida Fund kunufaisha wananchi

0
142


Mfuko wa Faida (Faida Fund) ni moja kati ya ajenda za maendeleo zinazoenda kuwanufaisha wananchi wa Tanzania.

Hayo yamesemwa na Dkt. Natu Mwamba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha katika hafla ya ufunguzi rasmi wa mfuko huo jijini Dar es Salaam.

Aidha, ameongeza kuwa Wizara ya Fedha itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kukuza uwekezaji nchini.

Dkt. Mwamba ni Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke wa wizara ya fedha na leo ni mara yake ya kwanza kuhutubia tangu aapishwe kushika wadhifa huo.

Kabla ya cheo hicho, aliwahi kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya nyadhifa nyingine nyingi.