EOTF yapata mafanikio makubwa miaka 25

0
103

Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Anna Mkapa amesema tangu kuanzishwa kwake hadi sasa, mfuko huo umewezesha wanawake kuuza bidhaa zenye thamani ya shilingi trilioni moja.

Amesema EOTF imeendelea kuwezesha wanawake, vijana na watoto katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu, afya na uchumi.

Mama Anna Mkapa amesema mfuko huo umesaidia sana katika sekta ya elimu ambapo watoto wengi hasa waliosaidiwa wamekuwa wasomi wakubwa wanaofanya kazi ndani na nje ya nchi katika taasisi na mashirika mbalimbali.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997, Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote umesaidia takribani watu elfu sita, wengi wao wakiwa wanawake wajasiriamali.