Elimu ya Sensa yaendelea kushika kasi

0
196

Kuelekea Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu wananchi wametakiwa kuonesha utayari na ushirikiano wao kwenye zoezi hilo ili kufanikisha azma ya serikali kuratibu mipango ya maendeleo kwa wananchi wote.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Amani Tanzania (TPF), Sadiq Godigodi mara baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam, hafla iliyoambatana na maandamano ya amani kwa ajili ya kutoa elimu ya kuhamasisha wananchi kutambua umuhimu wa kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi Kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku.

Pia, Godigodi amesisitiza suala la amani na utulivu kuzingatia wakati wa zoezi la sensa likiendelea ili kila mwananchi aweze kupata haki yake ya msingi ya kuhesabiwa pasi usumbufu wowote.