Elimu ya mpigakura kutolewa kwa kuzingatia haki

0
268
Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng'wanakilala

Shirika la Legal Services Facility (LSF) linalojishughulisha na upatikanaji haki kwa raia wote kupitia uwezeshaji wa kisheria nchini limewataka wadau wa mbalimbali wa uchaguzi kutumia ipasavyo ruzuku walizopewa katika kutoa elimu ya mpigakura kwa raia wote hususani wanawake kwa kuzingatia haki.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya utoaji wa elimu ya mpigakura na uraia kwa wadau wa uchaguzi ikiweo wadau wa maendeleo DANIDA, Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakilala amesema shirika hilo limeamua kutoa mafunzo hayo kwa wadau wake waliopewa vibali na NEC ili kuwaongezea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao kwa mpiga kura.

Baadhi ya wadau waliopata mafunzo hayo wameeleza namna walivyojipanga kuwafikia wananchi wengi kwa haraka zaidi katika kutambua haki yao ya msingi kuelekea uchaguzi mkuu.

“Tunaamini fursa hii ya kupata mafunzo haya yataleta tija kwenye jamii katika kufanya maamuzi sahihi ya kuwachagua viongozi wanaowataka”

Zaidi ya mikoa 17 nchini ikiwemo Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Unguja Kusini na Mjini Magharibi inatarajiwa kufikiwa na mashirika 31 kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.