Katibu Mkuu wizara ya Afya Profesa Abel Makubi ametoa wito kwa wananchi kuachana na mila na desturi potofu kuhusu hedhi.
Profesa Makubi amesisitiza juu ya upatikanaji wa huduma na vifaa vya kujihifadhi hasa taulo za kike sehemu zote kwa makundi yote kwa bei nafuu katika jamii.
Amesema hayo wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani.
Profesa Makubi amesema bado jamii ina uelewa mdogo kuhusu suala la hedhi, na kusisitiza ushirikiano katika mapambano dhidi ya mila na desturi potofu kuhusu suala la hedhi.
“Bado jamii yetu ina uelewa mdogo kuhusu suala la hedhi hivyo nitoe wito kwa jamii kuachana na mila na desturi potofu kuhakikisha upatikanaji wa huduma na vifaa vya kujihifadhi hasa taulo za kike sehemu zote kwa makundi yote na hata kuwa na bei elekezi katika bidhaa hii.”amesema Profesa Makubi
Amesema wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau inaendelea kutoa elimu na uhamasishaji kwa jamii ili kuongeza ufahamu juu ya masuala ya hedhi salama.
