EACOP mambo safi

0
127

Wakazi wa kijiji cha Njoro kata ya Kibaya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara wameishukuru serikali kwa kuendeleza mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga.

Wakizungumza na mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakazi hao wamesema, wako tayari kuchangamkia fursa za ujenzi katika mradi huo.

Mwalimu Clemenciana Shayo ni miongoani mwa watu waliopisha mradi huo na kulipwa fidia ambaye amesema kuwa, ameridhika nayo na anafurahi mradi huo kupita kijijini kwao kwani utafungua fursa mbalimbali.

Kwa upande wake mkuu wa wlaya ya Kiteto, Mbaraka Batenga amesema, elimu imeshatolewa kwa wananchi juu ya fursa zinazopatikana katika mradi huo wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki.

Amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo imeendelea kijiimarisha katika ulinzi wa bomba hilo kuanzia hatua za awali na utakapoendelea.

Bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga lina urefu wa kilomita 1,447 na hadi kukamilika kwake ujenzi wake unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi trilioni 11.