Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga amekabidhi kwa serikali mali zilizotaifishwa kutokana na kesi mbalimbali, ikiwa ni hatua ya kutunza rasilimali za Taifa na kulinda mali za umma.
Akikabidhi mali hizo zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 19 jijini Dar es salaam, Mganga amesema kuwa mali zilizotaifishwa na kukabidhiwa kwa serikali ni pamoja na madini, nyumba na magari.