DP WORLD INA UTAALAMU MKUBWA

0
150


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Kampuni ya DP World imeonesha kuwa na utaalamu, teknolojia, uwezo na uzoefu mkubwa katika uendeshaji wa bandari 190 katika nchi 68 barani Afrika, Asia, Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kusini.

Aidha, amewatoa hofu wananchi kuwa wakati wote wa utekelezaji wa makubaliano hayo na mikataba itakayoingiwa, vyombo vya Ulinzi na Usalama vitaendelea kutekeleza majukumu yao katika eneo la mradi kama vilivyofanya katika kipindi cha miaka yote 22 ya mkataba na mwekezaji wa awali (TICTS) aliyemaliza mkataba wake mwezi Novemba, 2022.