Dozi nyingine ya chanjo yawasili

0
148

Tanzania leo imepokea msaada wa dozi laki tano za chanjo dhidi ya UVIKO –  19 aina ya Sinopharm kutoka nchini China.
 
Akizungumza wakati wa mapokezi ya dozi hizo za chanjo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Abel Makubi amewataka Watanzania ambao tayari wamepata chanjo ya Sinopharm kuhakikisha wanapata dozi mbili kama inavyoelekezwa.
 
Amesema ili uweze kupata kinga inayotakiwa dhidi ya UVIKO – 19,  kwa chanjo ya Sinopharm  ni lazima upate dozi zote mbili.
 
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  hadi kufikia Oktoba 31 mwaka huu  Watanzania 88,546 walikuwa wamepata chanjo ya Sinopharm.