Dkt. Tulia kuwania Uspika

0
141

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, ni miongoni mwa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliojitokeza kuchukua fomu kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya kiti cha Spika wa Bunge hilo.

Dkt. Tulia amechukua fomu hiyo kwenye ofisi za CCM Makao Makuu Dodoma.

Chama cha Mapinduzi kimetangaza mchakato wa kupatikana kwa mgombea wa nafasi ya kiti cha Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo zoezi la uchukuaji wa fomu linafanyika kuanza hii leo hadi tarehe 15 mwezi huu kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Makao Makuu Dodoma, Ofisi ndogo ya CCM Lumumba na Kisiwandui Zanzibar.

Mchakato wa kupata Spika mpya unafanyika baada ya aliyekuwa Spika Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo tarehe sita mwezi huu.