Dkt. Tulia akutana na Spika wa Indonesia

0
252

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Dkt. Puan Maharani katika ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia, wakati wa mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Katika mazungumzo yao, wamekubaliana kuenzi na kuimarisha ushirikiano baina ya Mabunge ya Tanzania na Indonesia na kuongeza nguvu ya ushawishi na kuwajengea uwezo Wanawake wengi zaidi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kuleta usawa wa kijinsia.