Bendera kupepea nusu mlingoti kwa siku tatu

0
2340

Rais Dkt. John Magufuli ameagiza kuanzia kesho bendera za serikali kupepea nusu mlingoti kwa siku tatu hadi Septemba 24 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dodoma kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ameagiza watu wote wanaohusika na shughuli za uendeshaji wa kivuko cha MV Nyerere kukamatwa na kuhojiwa na watakaokutwa na hatia wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Aidha Balozi Kijazi amebainisha kuwa mpaka sasa watu 127 wamekufa katika kivuko hicho.