Dkt. Samia : Umoja na mshikamano ndio nguzo

Mkutano Mkuu wa 10 wa CCM

0
115

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza Umoja na Mshikamano ndani ya chama hicho pamoja na Jumuiya zake.

Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa 10 wa CCM unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.

Amesema Umoja na Mshikamano ndani ya CCM ndio njia pekee ya kukiwezesha chama hicho kufanikisha malengo yake hasa katika kuisimamia serikali ili iweze kuwaletea wananchi maendeleo.

Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa pia amesisitiza suala la kukiimarisha chama ili kiendelee kuwa imara na kuendelea kuwa miongoni mwa vyama vikubwa na vyenye nguvu Barani Afrika.

Ametumia mkutano huo kuwapongeza viongozi wote wa CCM na Jumuiya zake waliohudumu kipindi cha miaka mitano iliyopita, kwa kusema kuwa wamefanya kazi nzuri katika kukijenga na kukiimarisha chama.

Amewataka viogozi wa CCM ambao tayari wamechaguliwa na ambao watachaguliwa katika mkutano mkuu wa 10 wa chama hicho kufanya kazi zaidi ya ile waliofanya watangulizi wao ili chama kiwe imara zaidi.