Dkt. Samia: Tunalijenga upya Taifa letu

0
97

Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mwelekeo wa Serikali yake ni kuhakikisha taifa la Tanzania linarudi kwenye misingi iliyowekwa na waasisi wake na kuwika kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Rais Samia pia amesema mwelekeo huo unachagizwa na maridhiano ambayo yamefikiwa baina ya vyama vya siasa na mazungumzo yanayoendelea yanatoa mwanga wa kufikia mafanikio hayo.

Akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Dkt. Samia amesema, maridhiano ndio nguzo kuu ya kulijenga taifa katika misingi ya masikilizano na maelewano ili kujenga amani na utulivu wa taifa.

Amesema amani na utulivu uliopo hapa nchini unatokana na maridhiano na masikilizano yanayoendelea baina ya vyama na vyama na serikali.