Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaenda kuukwamua mchakato wa mabadiliko ya katiba ili kuangalia mapungufu na kuboresha baadhi ya mambo kwenye katiba ya sasa.
Akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Dkt. Samia amesema, mchakato huo utafanywa na kamati maalum itakayojumuisha wanasiasa na watu wengine wasio wanasiasa ili kupata uwakilishi wa pande zote.
Rais Samia amesema, kamati hiyo itaangalia namna ya kuboresha katiba ya sasa kwa kuzingatia pia mapendekezo ya tume ya Warioba ya mwaka 2014 na mapendekezo yaliyotolewa na kikosi kazi.
Amesema mapendekezo yatakayotolewa lazima yazingatie mila na desturi za Watanzania kwani sio kila haki inaweza kuwa sawa baina ya Taifa moja na linguine.