Dkt: Samia: Tulinde maadili ya watoto wetu

0
188

Rais Samia Suluhu Hassan amewaasa wazazi na walezi nchini kutenga muda wa kuwapa malezi watoto wao, ili kuondokana na janga la vijana wengi kuiga tamaduni zisizofaa kwa jamii.

Rais Samia amewataka wazazi na walezi kutokubali watoto waharibikiwe kwa kisingizio cha kukosa muda wa kuwapa malezi, ili kuinusuru jamii na vizazi vijavyo.

Ameongeza kuwa utamaduni wa Mtanzania lazima ulindwe na kamwe Tanzania haitakubali kupokea ama kurithi tamaduni zisizofaa kwa wananchi wake.

Rais Samia amewataka Waumini wa dini ya Kiislamu kutumia mafunzo waliyoyapata wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, yanayosisitiza kustahimiliana na kupendana.