Dkt. Samia: maridhiano yanatufanya tuishi kwa upendo

0
158

Rais Samia Suluhu Hassan amesema amani, utulivu na furaha inayoonekana kwa Watanzania wa makundi mbalimbali hasa Wanasiasa, inatokana na maridhiano ambayo yamefikiwa baina ya vyama vya siasa hapa nchini.

Rais Samia amesema, haikua rahisi kuona viongozi wa vyama vya siasa wakikaa pamoja kwa mioyo safi na furaha kama ilivyo sasa ambapo kila mmoja anafurahia kushirikiana na wengine.

Akizungumza katika Baraza la Eid El Fitri Kitaifa lililofanyika mkoani Dar es Salaam Rais Samia amesema, anajisikia fahari kuona viongozi wa kidini na wale wa kisiasa wanakaa kwa pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali.

Amewaasa Watanzania kuendelea kujizuia kufanya maovu kama ilivyokuwa wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma, ili yale yote yaliyokusudiwa wakati wa funga yawe na heri katika maisha ya kila siku.