Dkt. Samia awasili Ethiopia

0
230

Rais Samia Suluhu Hassan yupo nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa 36 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa leo Februari 16, 2023, Dkt. Samia
amekagua gwaride la heshima.

Pia amepata fursa ya kuangalia ngoma za asili za Taifa la Ethiopia kwenye uwanja huo wa ndege wa Kimataifa wa Bole.