Dkt. Samia aomboleza kifo cha balozi Mushi

0
89

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na kifo cha Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushi.

Dkt. Samia amesema Tanzania imeondokewa na Mwanadiplomasia mahiri na mtumishi makini wa umma.

Balozi Mushi pia alikuwa mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika mashirika ya Kimataifa Vienna, Austria.