https://www.youtube.com/watch?v=9qhZEZglR7w
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayub Rioba amesema wakati umefika kwa vyombo vya habari vya Afrika kuandika mambo mazuri yanayofanywa Barani humo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya mkutano wa 39 wa Mawaziri wa Uchukuzi, Mawasiliano, TEHAMA na Hali ya Hewa unaofanyika jijini Dar es Salaam, Dkt Rioba amesema kuwa, sasa ni wakati kwa vyombo vya habari kuandika mambo mazuri yanayofanywa Barani Afrika.
Dkt Rioba amesema kwa sasa Afrika ina mambo mengi mazuri ya kutangazwa na vyombo vya habari, hivyo lazima vibadilike na viache kuandika habari zenye mlengo hasi na Afrika.
Kuhusu maendeleo ya teknolojia na uwepo wa mitandao ya kijamii, Dkt Rioba amesema kuwa ni lazima itumike vizuri kuhabarisha jamii na kujiepusha na kutangaza habari za uongo.