Dkt. Rioba aridhishwa na ujenzi Serengeti

0
190

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha ameeleza kuridhishwa na marekebisho yaliyofanywa na Mkandarasi kampuni ya Caliber First Group anayetekekeza ujenzi wa miundombinu ya kituo kipya cha mitambo ya kurushia matangazo ya redio ya TBC Taifa na TBC FM huko Mugumu wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Juni 08, 2023 alipokagua ujenzi huo Dkt. Rioba alieleza kutoridhishwa kutokana na kituo hicho kujengwa chini ya kiwango ikiwa ni pamoja na vigae ambapo kwa sasa vimeondolewa na kuwekwa vingine.

Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Caliber First Group Faraj abdala amekiri hapo awali ujenzi huo kuwa na dosari na kuongeza kuwa ameshachukua hatua ya kumsimamisha kazi msimamizi aliyekuwa akisimamia ujenzi wa vituo vipya vitano vya mitambo ya kurushia matangazo ya TBC katika maeneo mbalimbali nchini.