Katibu Mkuu MstaafuuDkt. Laurien Ndumbaro amesema moja ya mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai ni kuwepo na staha kwenye ukaguzi wa wafungwa, kwani hali ilivyo sasa Jeshi la magereza wanatweza utu wa wafungwa.
Dkt. Ndumbaro amesema ukagguzi wa wafungwa unahusisha wafungwa kuvuliwa nguo zote na kubakia utupu mbele za wafungwa wengine na hivyo kuondoa haki ya ulinzi wa faragha ya wafungwa na kutweza utu wao.
“Moja kati ya mambo ambayo wafungwa wametueleza tukamwambie Rais ni kwamba wao pia ni Watanzania na wana haki ya kulindwa utu wao. Hali ilivyo sasa askari Magereza wanawaadhibu wafungwa badala ya kuwapa mafunzo,” Amesema Dkt. Ndumbaro