Dkt. Ndugulile : Tozo zifutwe

0
120

Mbunge wa jimbo la Kigamboni mkoani Dar es Salaam Dkt. Faustine Ndugulile ameiomba wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kufuta tozo katika daraja la Kigamboni ili kuwapunguzia gharama wananchi wa maeneo hayo kwa kuwa pia wanachangia katika ujenzi wa madaraja mengine nchini.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Pia Dkt. Ndugulile ameshauri kuwa madaraja mengine kama la Tanzanite yasiwekewe tozo.