Dkt. Nchemba : Tumieni huduma za kibenki

0
313

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania kutumia huduma za kibenki badala ya kuweka fedha zao kwenye taasisi bubu.

Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la CRDB ambalo ndilo makao makuu ya benki hiyo.

Amesema huu ni wakati wa Watanzania kutumia huduma za kibenki bila woga, kwa kuwa kuna usalama wa pesa zao.

Pia Dkt. Nchemba amezungumzia uwepo wa watu wasio waaminifu kwenye mikopo yao wanayokopa benki, jambo linalokwamisha ufanisi wa huduma hizo kwa wateja wengine.

“Naomba kusisitiza hapa ndugu zangu Watanzania kumekuwa na watu wasio waaminifu kwenye mikopo hasa Wanaume wakikopa wagumu kufanya marejesho hasa mke wake akiwa hajui, Wanawake wamekuwa wakijitahidi kurejesha mikopo kuliko Wanaume, niombe sana tujitahidi kurejesha mikopo tunayochukua.” Dkt Nchemba

Aidha amesema kuwa uchumi wa nchi umezidi kuimarika kutokana na usimamizi mzuri wa Serikali na kusisitiza weledi kwa baadhi ya watumishi wa mabenki wanapokuwa wanawahudumia wateja wao hasa katika eneo la mikopo.