DKT. MWINYI: TUNATAMBUA MCHANGO WA WAHANDISI

0
207

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema Serikali inatambua mchango wa taaluma ya uhandisi wa fani mbalimbali katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia huduma mbalimbali.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokuwa akifungua Kongamano la nane la Wahandisi Wanawake Tanzania (TAWECE).

Aidha, Rais Mwinyi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha wanaongeza idadi ya wahandisi hasa Wanawake na mafundi sanifu.

Ameongeza kuwa Serikali itahakikisha inawasaidia Wasichana wanaosoma masomo ya Sayansi katika elimu ya Sekondari, Vyuo vya mafunzo ya amali na Vyuo Vikuu katika hatua ambayo itasaidia kuongeza idadi ya Wahandisi Wanawake nchini.