Dkt. Mpango: Tudumishe amani na mshikamano

0
372

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewaomba Viongozi wa dini nchini kuendelea kuimarisha uhusiano baina yao na Waumini, ili kudumisha amani, umoja na mshikamano uliopo.

Dkt. Mpango alikuwa akizungumza wakati wa futari maalum iliyoandaliwa na Kamati ya amani ya mkoa wa Dar es salaam katika viwanja vya Karimjee.

Amewataka Viongozi hao wa dini kukemea matendo ya kikatili, ukatili wa kijinsia, mapenzi ya jinsia moja, dhuluma pamoja na rushwa.

Kwa Waumini wa dini ya Kikristo amewatakia maandalizi mema ya Sikukuu ya Pasaka ambayo itasherehekewa tarehe tarehe 17 mwezi huu.

Aidha Makamu wa Rais amewatakia Waumini wote wa dini ya Kiislamu mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.