Dkt. Mpango : TRA msiwanyanyase wafanyabiashara

0
178

Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango, ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutowanyanyasa wafanyabiashara badala yake wazingatie sheria na weledi katika kukusanya kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Dkt.Mpango ametoa kauli hiyo wakati akitoa salamu za Pasaka mwaka 2021, katika Kanisa Kuu Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma lililopo Jijini Dodoma.

” Ninataka kodi kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania, TRA msiwanyanyase wafanyabiashara”, amesema Dkt.Mpango.

Pia amewahimiza Watazania kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kama sehemu ya kumuenzi hayati Dkt.John Magufuli ambaye alihimiza watu kufanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya kuinua uchumi wa Taifa.

“Kazi zote njema ni kazi ya Mungu hivyo tunao wajibu wa kufanya kazi kwa nguvu zetu zote ili tumrudishie Mungu shukurani”, ameongeza Dkt.Mpango.