Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewaonya wakulima nchini wanaopima mazao kwa kutumia Rumbesa na kuwataka kutumia mizani katika kupima mazao hayo.
Dkt. Mpango ametoa onyo hilo alipokuwa akifungua rasmi maonesho na sherehe za sikukuu ya wakulima (Nanenane) kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Pia ameagiza uuzaji wa mifugo katika minada ufanyike kwa kutumia mizani huku akizielekeza halmashauri nchini kutotumia faini za Rumbesa kama chanzo cha mapato.
Kwa upande wa wizara ya Kilimo, Makamu wa Rais ameiagiza kushirikiana na wizara nyingine kuendelea kuweka majokofu katika viwanja vya ndege ili kuhifadhi mazao yanayoharibika haraka pamoja na kuanzisha viwanda vya kusindika mazao hayo.