Dkt. Mpango: Riba ya mikopo bado mzigo

0
75
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi na washiriki mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa inayofanyika katika Viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza. Tarehe 24 Novemba 2022.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa watoaji wa huduma za kifedha nchini kutazama upya masharti ya mikopo ikiwemo dhamana ya mali zisizohamishika kwa kuwa ni kikwazo kwa wajasiriamali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo juu utendaji wa Benki Kuu kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu Nchini Profesa Florens Luoga wakati alipotembelea Banda la Benki hiyo wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa inayofanyika katika Viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza. Tarehe 24 Novemba 2022.

Pia amewataka kutafuta njia za kibunifu katika kuwafikia vijana nchini, ili waweze kupata mikopo itakayoinua maisha yao na uchumi wa Taifa.

Makamu wa Rais amesema hayo jijini Mwanza wakati akifungua maadhimisho ya pili ya wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha kutoka Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Ramia Rashid Ramia wakati alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Ufunguzi wa Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa inayofanyika katika Viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza. Tarehe 24 Novemba 2022.

Amesema riba ya mikopo ya wastani wa asilimia 16 bado ni mzigo kwa Watanzania wengi, hivyo amesisitiza kila benki kupitia umoja wao kuchambua mizizi ya changamoto hiyo na kupunguza zaidi riba kwa wakopaji.

Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa wito kwa watoaji huduma za kifedha nchini kupunguza gharama za kutuma na kupokea pesa kimataifa kwa kuwa zimekuwa zikisababisha wageni pamoja na Diaspora kutumia njia zisizo rasmi.

Pia ameutaka Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) kusaidia kuhamasisha wanachama wao kutanua wigo wa huduma za kifedha katika maeneo ya vijijini.