Dkt. Mpango : Msitumie watoto kujinufaisha

0
160

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema haridhishwi na usimamizi wa baadhi ya taasisi zinazotunza wototo, na kuzitaka taasisi zinazotumia Watoto kujinufaisha ziache mara moja.
 
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo mkoani Dodoma wakati akizindua Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo Kikombo, uzinduzi uliofanyika pamoja na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambayo hufanyika Juni 16 kila mwaka.
 
Amesema si jambo la uungwana kwa baadhi ya taasisi kutumia kigezo cha kutunza Watoto kujinufaisha badala ya kuwalea Watoto hao kama ilivyoainishwa katika malengo ya kuanzishwa kwa
taasisi hizo.
 
Makamu wa Rais pia ametoa wito kwa Wadau wote wanaohusika na malezi ya Watoto kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutoa elimu juu ya haki na ustawi wa mtoto.
 
Dkt. Mpango amesisitiza  kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali katika kusaidia watoto walio katika mazingira magumu, na amelipongeza shirika la ABBOT Fund Tanzania kwa ushiriki wao katika ujenzi wa Makao ya Taifa ya Watoto.
 
Ujenzi wa Makao hayo ya Taifa ya Watoto umegharimu shilingi bilioni 12.7.