Dkt. Mpango amjulia hali Dugange

0
231

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange leo Aprili 29, 2023, alipofika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa, Dodoma kumjulia hali baada ya kupata ajali ya gari.

Dkt. Dugange alipata ajali usiku wa Aprili 26, 2023 wakati akiendesha gari yake binafsi jijini Dodoma.

Kwa sasa Dkt. Dugange anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa.