Dkt. Mpango akagua miradi Buhigwe

0
259

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, inayotekelezwa katika wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ule wa ujenzi wa barabara ya Buhigwe – Muyama – Kasumo.

Dkt. Mpango amesema barabara hiyo ni jitihada za Serikali katika kuufungua mkoa wa Kigoma na kuunganisha na mikoa mingine pamoja na nchi jirani, na hivyo kuchochea biashara na ukuaji wa uchumi kwa Wananchi.

Akiwa wilayani Buhigwe, Makamu wa Rais pia amekagua ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kasumo na nyumba za wahudumu wa afya wa zahanati hiyo, ,mradi unaotekelezwa kwa nguvu za Wananchi kwa kushirikiana na Serikali.

Amewapongeza wananchi wa Kijiji hicho kwa kujitolea kuongeza eneo la zahanati hiyo pamoja na kutoa mchango wa hali na mali katika utekelezaji wa mradi huo na kuwaomba waendelee kutoa mchango katika miradi mingine.