Dkt. Mpango ahimiza nguvu zaidi kwa watoto njiti

0
194

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa wadau, taasisi za dini pamoja na wananchi kwa ujumla kulipa kipaumbele suala la kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ili kukabiliana na changamoto ya vifo vinavyotokana na hali hiyo.

Amesema serikali imeendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kwa ujenzi wa hospitali za wilaya, vituo vya afya katika kata pamoja na zahanati katika vijiji ili kuendelea kukabiliana na changamoto za vifo vya mama na mtoto.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, mara baada ya Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 25 Julai 2022.

Ametoa rai hiyo akizungumza na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti), Doris Mollel, Mazungumzo na kumsihi kuwekeza katika utoaji elimu ya afya ya uzazi ili kukabiliana na ongezeko la watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwani maeneo mengi hasa ya vijijini wanashindwa kupata uelewa juu jambo hilo.

Kwa upande wakeMollel amempongeza Makamu wa Rais kwa jitihada alizofanya za kutambua changamoto zinazojitokeza katika malezi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati hapa nchini na kuamua kuchangia vifaa tiba kwa ajili ya watoto hao katika hospitali ya taifa Muhimbili hivi karibuni.

Amesema tayari serikali imetenga shilingi bilioni 23.36 katika bajeti ya Wizara ya afya kwa mwaka 2022/2023 pamoja na kutenga vyumba mia moja kwaajili ya watoto njiti ili kuweza kupunguza idadi ya watoto njiti wanaopoteza maisha kutokana na changamoto mbalimbali.