Ubunifu kwenye uandaaji na uwasilishaji wa habari umetajwa kama moja ya nyenzo muhimu katika chombo chochote cha habari.
Hayo yamesemwa na Dkt. Egbert Mkoko ambaye ni miongoni mwa majaji wa shindano la Utangazaji na uandaaji wa habari kwa Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya habari vilivyopo mkoani Dar es Salaam, lililoandaliwa na TBC FM.
Dkt. Mkoko ametoa rai kwa Wanafunzi wa uandishi wa habari nchini kutanguliza ubunifu mbele, ili waendane na soko la habari.