Dkt Matonya: Watanzania tujitokeze kuhesabiwa

0
216

Watanzania wametakiwa kuendelea kujiandaa na siku ya sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka huu ili Serikali iweze kupanga Bajeti yake kwa usahihi kulingana na idadi halisi ya watanzania.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kikristo Tanzania (CCT) Dkt Moses Matonya wakati akitoa Salamu za CCT kwenye Ibada ya Pasaka Kitaifa iliyofanyika katika Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Morogoro mjini na kuongeza kuwa zoezi la kuhesabu watu na makazi litasaidia Kurahisisha kujua idadi halisi ya watu ili kupanga Bajeti ya Serikali.

Dkt Matonya ameongeza kuwa mwaka huu kumekuwa na mvua isiyo ya uhakika hivyo amewakumbusha watanzania kutunza chakula kilichopo na kulima vyakula vinavyohimili aina ya mvua za mwaka huu ili mwakani nchi isiingie kwenye janga la njaa na uhitaji wa chakula.

Katika Salamu hizo, Dkt Matonya ameongeza kuwa watanzania wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhali ya ugonjwa wa UVIKO-19 ambao bado upo na kuwasihi watanzania kuacha kupuuza kuchukua tahadhali za ugonjwa huo ili kuepukana na vifo kwa watanzania.