Dkt. Mahenge aagiza wakurugenzi kushiriki ziara zake

0
100

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya mkoani humo kuhudhuria ziara zake anazozifanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi, badala ya kutuma wawakilishi.

Dkt. Mahenge ametoa agizo hilo baada ya kupata taarifa kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba, Mhandisi Michael Matomora hayupo kwenye mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Misigiri kilichopo wilayani Iramba kilicholenga kusikiliza kero zao.

Wakati wa mkutano huo Dkt. Mahenge amehoji kulikuwa na ulazima gani kwa mkurugenzi huyo wa halmashauri ya wilaya ya Iramba kwenda kuhudhuria mkutano wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) badala ya kutuma mwakilishi ili uey ashiriki kwenye ziara hiyo.

Amesema yeye ni mwakilishi wa Rais, hivyo kero za wananchi rais atazipata moja kwa moja kwa sababu wananchi wana haki ya kumweleza kero zao.