Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Jumanne, Januari 14, 2020 anatarajia kuwaapisha mabalozi wateule wanne watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.
Wanaotarajiwa kuapishwa ni:
- Meja Jenerali (MST) Gaudence Milanzi, atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Africa Kusini
- Dkt. Modestus Francis Kipilimba, atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Namibia
- Prof. Emmanuel David Mwaluko Mbennah, atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe
- Dkt. Benson Alfred Bana, atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria