Dkt. Kikwete: CCM inafaa kuendelea kuongoza nchi

0
655

Rais Mstaafu wa wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kinafaa kuendelea kupewa ridhaa ya kuongoza nchi kutokana na kuwa na sifa bora za kuongoza.

Akihutumia katika mkutano wa kampeni Mbagala jijini Dar es Salaam amesema CCM ina sifa zote za uongozi kutokana na kuwa na sera bora inayowaunganisha Watanzania katika misingi ya amani, upendo, umoja na mshikamano huku ikiweka mbele vipaumbele vya kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo.

Dkt. Kikwete amewataka wananchi kumchagua mgombea wa urais wa CCM, Dkt. John Magufuli aendelee kutekeleza miradi ya kuwaletea maendeleo wananchi pamoja na kutatua kero zinazowakabili ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi ikiwemo rushwa na nidhamu mbovu ya watendaji wa umma katika kutoa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake (UWT), Gaudencia Kabaka na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba amewasihi wananchi kushiriki kupiga kura na kuchagua wagombea wa CCM.

Wananchi wa Temeke wametakiwa kushiriki kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao kwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wananchi wengi wilayani humo walijiandikisha kupiga kura ila hawakushiriki kupiga kura.