Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuna umuhimu wa kufanya tafiti kujua ni kwa nini idadi ya wahitimu wanaume katika chuo hicho imekua ikipungua mwaka hadi mwaka.
Dkt. Kikwete ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa mahafali ya 52 duru ya tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ameyasema hayo baada ya taarifa ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye kueleza kuwa, kati ya wahitimu wote wa chuo hicho kwa mwaka huu ambao ni zaidi ya elfu 11 , asilimia 51 ni wanawake.
Alisema kuwa katika mwaka wa masomo wa 2022/2023 kati ya wanafunzi wote waliodahiliwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, asilimia 53 ni Wanawake.
Dkt. Kikwete amesema jambo hilo si la kufumbia macho, kwani linaweza kwa na athari katika siku zijazo.