Dkt. Kijazi: Tupo katika majonzi makubwa

0
376

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi ambaye ni mdogo wa marehemu, Balozi John Kijazi amesema kuwa kipindi hiki ni cha majonzi sana kwao kwani hivi karibuni walimpoteza kaka yao mkubwa.

Dkt. Kijazi ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa TANAPA ameishukuru serikali kwa namna ambavyo imekuwa pamoja nao tangu kuugua kwa ndugu yao, kufariki, hadi hatua iliyofikia sasa ambapo utazikwa leo Korogwe mkoani Tanga.

Amewashukuru Watanzania kwa namna wamekuwa faraja kwa familia katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Akieleza ratiba ya mazishi, amesema itaanza 3:00 asubuhi na mwili wa marehemu utawekwa katika nyumba yake ya milele saa 8 mchana.

Misa Takatifu ya mazishi itafanyika katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Augustino na itaongozwa na Mhashamu Askofu Telephore Mkude.