Dkt. Kalemani Tanzania ya kwanza kuendesha Treni kwa umeme Afrika Mashariki

0
231

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuwa na treni inayotumia umeme (electric train)

Dkt. Kalemani ameyasema hayo eneo la Kingolwira, Morogoro wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi maalum wa Kusafirisha umeme utakaotumika katika reli ya kisasa ya (SGR).

“Nchi ya Tanzania itakuwa ni nchi ya kwanza Afrika Mashariki na ya sita Afrika kwa kuendesha treni ya mwendo kasi inayotumia nishati ya umeme na hivyo kurahisisha na kuchochea kasi ya ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii”, amesema Dkt. Kalemani.

Kalemani ameongeza kuwa, katika kutekeleza miradi ya huduma wezeshi kwa mradi wa SGR, tayari Wizara ya Nishati kupitia TANESCO wako katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi mahususi wa kusafirisha umeme kwa ajili ya kuendesha treni hiyo.

Aidha, awamu ya kwanza ya utekelezaji kutoka Dar es salaam hadi Morogoro, yenye urefu wa kilomita 161 umekamilika kwa asilimia 94.