Dkt. Elia na juhudi za kukuza Kiswahili

0
61

Mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Lulu za Kiswahili cha TBC I Dkt. Victor Elia ametoa rai kwa vyombo vya habari nchini kuongeza wigo katika kuitangaza na kuikuza lugha ya Kiswahili, ikiwa ni pamoja na kuanzisha vipindi mbalimbali vyenye muktadha wa lugha hiyo.

Dkt. Victor ametoa rai hiyo mkoani Dodoma alipokuwa akizungumza katika kongamano la Kiswahili la miaka 61 ya Uhuru.

Amesema kuna hali ya kutotambua mchango wa vyombo vya habari nchini katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili, hivyo ni vema wadau wakaliangalia jambo hilo ili mchango wa vyombo hivyo uweze kutambuliwa.