Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Zainab Chaula ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi mkoani Mwanza, ameelezea kuridhishwa na ujenzi unaoendelea wa maabara pamoja na jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya cha Buzuruga wilayani Ilemela.
Dkt Chaula anaendelea na ziara yake mkoani Mwanza, ziara yenye lengo la kukagua ujenzi wa vituo vya afya, hospitali za wilaya pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.